simbadeo2000

Road to Kisarawe…

kisarawe22-4

Huu ndio mkeka wa kuelekea Kisarawe. Ni kiasi cha km 40 hivi kutoka katikati ya jiji la Dar es Salaam. Zamani safari ilichukua saa kadhaa, siku hizi ni safari ya dakika kadhaa tu. Ni mji mzuri kuutembelea. Umezungukwa na Msitu mnene wa Kazimzumbwi. Una madhari nzuri na ni eneo la juu ya milima. Kutoka Kisarawe unaweza kuona baadhi ya maeneo ya jiji la Dar, hasa yale yanayopakana na ufukwe wa Bahari ya Hindi.

Hali ya maisha haitofautiani sana na Dar.  Bei za bidhaa ni kama ilivyo pale Dar. Maji ndiyo tatizo kubwa kwa wakazi wa Kisarawe. Hata hivyo kuna juhudi kadhaa kujaribu kurekebisha hali hiyo.

kisarawe1-6

Ni moja ya jengo la zamani lililo upande wa mbele katika moja ya shule kongwe nchini Tanzania ya Minaki. Hapa kuna historia. Historia inayostahili kutunzwa. Kuna viongozi wengi wazito waliopata kusoma hapa. Naamini wakiamua wanaweza kubadili mwonekano wa mazingira ya shule hii maarufu na iliyo katika mandhari mazuri sana. Tukumbuke tulikotoka. (mtaniwia radhi kwa mkao wa picha, ni katika hekaheka za kupata picha kutoka kwenye gari lililo kwenye mwendo).


Posted in Siasa na jamii

Ujumbe kutoka Kisarawe…

dscf0006

Sanaa ni Kazi. Sanaa ni Ajira. Sanaa ni Maisha. Sanaa ni Maendeleo. Tufanye sanaa kwa maarifa, juhudi na ubunifu wa hali ya juu ili kutokomeza maadui zetu wakuu watatu: ujinga, maradhi na umaskini. Kwa njia ya sanaa sote tunaweza – kuanzia watoto hadi wazee. Huu ni ujumbe kutoka kwa wakazi wa Kisarawe, mkoani Pwani.


Posted in Siasa na jamii

Kuku wa Amadori

dscf0010

dscf0011

Pichani ni kuku wenye uzito kati ya kilo 4 mpaka 6 wanaouzwa kwa Amadori eneo la Uwanja wa Ndege, Dar es Salaam. Bei ya kuku ni Sh. 14,000/= kwa kuku jike na 22,000/= kwa jogoo.

Ufugaji kwa njia bora za kisasa ni moja ya njia tunazoweza kutumia Watanzania kujikwamua kutoka kwenye umaskini. Kuna somo hapo la kujifunza.


Posted in Siasa na jamii

Merry Christmas and Happy New Year 2009

simba-class31

Ilikuwa tarehe 22 November 1990. Ndiyo kwanzatulikuwa tumekamilisha kufanya mitihani ya Taifa ya Kidato cha Nne. Tulifanya safari ya kukwea Mlima Kilimanjaro. Sote tuliokuwa katika kundi letu tulifaulu kufika kileleni, Uhuru Peak. Ilikuwa safari ngumu na yenye kutoa changamoto kubwa kwetu. Tuliweka nia thabiti na lengo la kufika kileleni. Tulifaulu.

Picha hii inanikumbusha kwamba katika maisha tunahitaji kuwa na malengo, tunahitaji kuwa na nia thabiti ili kuyafikia malengo hayo, tunahitaji kujitoa sadaka ili kufikia malengo hayo. Vilevile, inanikumbusha kwamba tuweke malengo yetu juu zaidi kwani tukifanya hayo niliyoeleza hapo TUNAWEZA kufikia lengo lolote tunalojiwekea.

Natumia fursa hii kuwatakia Heri na Baraka za X-mas 2008 lakini pia kuwatakia Watanzania wenzangu na wasomaji wa blogu hii Heri na Mafanikio katika Mwaka Mpya wa 2009.

Tukumbuke kwamba TUNAWEZA – tunaweza kubadili hali zetu kama Taifa, tunaweza kubadili maisha yetu kila mmoja kwa nafsi yake.

Pichani, kutoka kushoto: John Bosco Mosha, Furaha Massawe, Reginald Mbuya, Paul (Christian) Temu, Sylivester Kusare, Valentine Tesha, Straton Mushi, Kanut Bynit na mimi Deogratias Simba (aliyechuchumaa).


Posted in Siasa na jamii

On Zimbabwe – Military Intervention

simbastreetphotosoctnov2007-282

We need peaceful means of resolving the Zimbabwe crisis. Stop opting for violent means. We need peace. Save lives of children, women and the elderly. A political resolution is possible.

THREAT OF MILITARY INTERVENTION IN ZIMBABWE

 

We, the undersigned African scholars, are greatly concerned about threats of military intervention in Zimbabwe, ostensibly in the name of human rights and for humanitarian purposes. We fully recognize the political impasse in Zimbabwe and the resultant prolonged suffering of its people. For that very reason, we appreciate the regional initiative taken by SADC to resolve this impasse politically. We are of the view that the political process must be given the space and the opportunity to be resolved in a peaceful and democratic way. The political process is the only way to allow the people of Zimbabwe to arrive at a sustainable solution. We condemn the use of violence to short cut the political process. We call upon the political actors in Zimbabwe to seek a solution that does not subject its people to suffer the consequences of violence. The duty of Africans and states is to facilitate this process in the spirit of Pan-Africanism as an act of solidarity with the Zimbabwean people.

 

Experience shows that the inevitable consequence of military intervention to resolve social and political conflicts has been endless wars, as the Democratic Republic of Congo and Somalia clearly demonstrate. In all these military interventions millions of people have suffered. Women and children are the most affected. Military interventions exacerbate political and socio-economic crises and internal differences with profoundly detrimental and destructive regional implications. We recognize that threats of military intervention come from imperialist powers, and also through their African proxies. Its consequence will be continued domination of the African continent while dehumanizing its peoples.

 

Military intervention in Zimbabwe will militarise the whole of Southern Africa. In protesting against threats of military intervention in Africa we confirm the right of African peoples to a peaceful life and to social justice, and to self-determination, including the right to solve our own problems through peaceful means.

 

Signed by Professor Issa Shivji, Professor Samir Amin, and 200 other scholars attending the 12th Congress of CODESRIA.

 

Yaounde, Cameroon

10TH DECEMBER 2008

As published by:

www.pambazukanews.com


Posted in Siasa na jamii

Uhuru Day

dscf00141

 

dscf0016

Tanzania imeadhimisha miaka 47 ya uhuru wake leo. Juu ni mnara wa uhuru katika viunga vya mapumziko vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam. Chini ni uhaba wa habari juu ya Sikukuu ya Uhuru katika magazeti kwenye kurasa zao za mbele. Ni gazeti moja tu, la The Citizen, ndilo lililobeba habari ndogo juu ya siku hii muhimu kwa Taifa letu.

Yapo mengi ya kujiuliza. Umri wa miaka 47 ni  umri mkubwa. Je, Tanzania imesonga mbele au imerudi nyuma katika maendeleo yake na ya wananchi wake? Mpaka katikati ya miaka ya 70 tulikuwa na viwanda vinavyozalisha bidhaa mbalimbali: zana za kilimo, redio, nguo, viatu, baiskeli, vipuri na mambo kadha wa kadha. Leo hii viwanda hivyo havipo au vimekwishabinafsishwa na kubadilishiwa matumizi. Vingine vimekuwa mabohari tu na vingine vinafanya shughuli nyingine ambazo ni vigumu kuziunganisha na dira yetu ya maendeleo kwa ujumla.

Wakati huohuo, jeshi la watu wasio na ajira rasmi na zenye mwelekeo wa kuzalisha kwa ajili ya maendeleo yao na yale ya Taifa linazidi kuwa kubwa. Kila mwaka wanazalishwa vijana mamia elfu wasio na uhakika wa ajira ya kudumu. Kilimo tunazidi kukitupa mkono, elimu inazidi kuwa ‘bora elimu’ na si ‘elimu bora’, maradhi (UKIMWI, malaria, TB, na mengine mengi yanazidi kushamiri. Miundo mbinu bado ni kitendawili – usafiri wa reli, anga, barabara na hata majinibado ni wa ubora wa chini.

Tujiulize iweje badala ya kuendelea kuwa wazalishaji tunazidi kugeuzwa kuwa dampo la kuuzia bidhaa, tena zilizo nyingi zikiwa ‘feki’, hivi sisi Watanzania tunafanya nini? Au ndiyo tuseme sote tumelewa ‘harakati za kujitafutia’ utajiri kwa njia za haraka na za kijanjajanja?

Hima tuamke. Turejee tafakari ya Rais J.F. Kennedy: Jiulize umeifanyia nini nchi na si nchi inakufanyia nini. Mjenga nchi ni mwananchi na mbomoa nchi ni mwananchi.


Posted in Siasa na jamii

About author

I am a citizen of Tanzania. I live in Dar es Salaam, commercial city of Tanzania. I am an editor, particularly dealing with books as well as other publications and related activities: editing, translating, supervising design and layout, monitoring printing, warehousing and dissemination of the books. I am also an author: I write children's story books, school textbooks and adult books. I undertake translation tasks from English to Kiswahili and vice versa. I do book indexing, that is preparing an index for a professional book. Contact: kakasimba@gmail.com . Feel free to get in touch with me.

Search

Navigation

Categories:

Links:

Archives:

Feeds