simbadeo2000

Eid Mubarak

 

Nawatakia nyote Eid njema na yenye baraka tele. Iwe Eid ya kusoma vitabu na kunoa akili kupitia vitabu. Uwe mwanzo mpya kwetu sote kusoma vitabu. Kila la kheri.


Posted in Siasa na jamii

Eid-el-Fitr is around the corner…

Wakazi wa jiji la Dar es Salaam wajimwaga mitaani kufanya maandalizi ya sikukuu ya Eid-el-Fitri. Pichani ni wakazi hao wakifanya manunuzi ya nguo na viatu katika Mtaa maarufu wa Kongo jijini Dar. Kwa kawaida siku ya Jumapili huwa ni siku tulivu jijini Dar. Lakini Jumapili ya leo imekuwa tofauti. Ikiwa leo ni chungu 27 katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, zimebaki siku chache kabla mwezi hauajaandama kuashiria kumalizika kwa mwezi huu.

Tuungane sote kufanya kipindi hiki cha sikukuu na siku nyingine kuwa kipindi cha amani na utulivu.

Nawatakia wasomaji wote wa blogu hii Ramadhani njema na heri tele kwa sikukuu ya Eid-el-Fitr.


Posted in Siasa na jamii

Mawasiliano yanapokatika …

Imagine.

Gari linagonga nguzo mojawapo katika hizo. Nini yatakuwa madhara yake? Sina uhakika. Lakini haitashangaza kuona ajali hiyo inazaa ajali nyingine mbalimbali. Nyaya live za umeme zitakatika. Watembea kwa miguu wataathirika. Nyumba zinaweza kushika moto. Gari lenyewe litaharibika na huenda nalo likashika moto. Kwa ujumla kutakuwa na maangamizi ya maisha ya binadamu, kuteketea kwa mali na wengine kupata vilema vya maisha. Je, ni kweli hapa ‘ajali haina kinga’? Tanesco mko wapi? Tanroads mko wapi?

Picha hizi ni kutoka barabara ya Majumbasita kwenda Kinyerezi. Ni za tarehe 24 Septemba 2008.


Posted in Siasa na jamii

Kaboom! Kaboom! Ajali …

Tuesday 2nd September 2008, Nyerere Road, Quality Plaza Area, 1.15pm.

Tuwapo barabarani, tupunguze mawazo,

Hata kama tupo

Kwenye orodha ya EPA,

Tupunguze mawazo, tuwapo barabarani,

Ili tuepushe ajali zinazokwepeka.

Hakuna aliyeumia katika ajali hii. Gari lenye usajili namba T 988 ALF liligonga kwa nyuma gari namba T 931 ARU ambalo nalo liligonga gari la Civila Aviation Authority lenye namba STK 4641. Tukiwa makini barabarani tunaweza kuepuka ajali kama hizi.


Posted in Siasa na jamii

About author

I am a citizen of Tanzania. I live in Dar es Salaam, commercial city of Tanzania. I am an editor, particularly dealing with books as well as other publications and related activities: editing, translating, supervising design and layout, monitoring printing, warehousing and dissemination of the books. I am also an author: I write children's story books, school textbooks and adult books. I undertake translation tasks from English to Kiswahili and vice versa. I do book indexing, that is preparing an index for a professional book. Contact: kakasimba@gmail.com . Feel free to get in touch with me.

Search

Navigation

Categories:

Links:

Archives:

Feeds