As I upload this post, Ziggy Marley’s number ‘Love Is My Religion’ is playing. ALL WE NEED IS LOVE. Then there would be no such thing as war, terrosim, weapons of mass destruction, atrocity, ethnic cleansing, unfair and unequal elections, corruption, imperialism, nazism and all the evils whatever the name you brand them with.
All we need is LOVE. Understanding. Compassionate. Wisdom. Truth. Brotherhood. Let’s learn love from children. They are our greatest teachers when it comes to understanding others, to loving others, to being wiser than we are.
Yes, we can. KEEP ON DREAMING. Love is My Religion.
Hii pia ni Dar es Salaam. Ni eneo la Kifuru ambalo limegawanyika – sehemu moja ni upande wa Ilala, kata ya Kinyerezi, na sehemu nyingine ni Kinondoni, kata ya Kwembe. Mji unasogea kwa kasi. Baada ya miaka mitano eneo hili litakuwa tofauti kabisa na linavyoonekana hivi leo. Ndiyo kusema, watu huleta maendeleo katika eneo mara nyingi wakiitangulia serikali na taasisi zake. Wawekezaji wa Kitanzania wanakaribishwa kuwekeza huku.
New House along Nyerere Road. Jamana House. The street is now richer with this newly born baby around. It is an important investment into the country. Keep it up Jamana.
Kutokea maeneo jirani na Kikosi cha Nyumbu tunaweza kuona jengo la Benki ya NMB Kibaha kwa mbali. Vinginevyo, jengo hilo huwa ni kivutio kikubwa katika ukanda huu. Ili kufika eneo picha ilipopigwa, unaingia ndani pale Kibaha kwa Mathias. Mkono wa kulia kama unatoka Dar.
Hospitali ya Tumbi, Kibaha. Ni wakati sasa wadau mbalimbali tushiriki kuiboresha hospitali hii muhimu. Sidhani kama tunahitaji mtu asisitize umuhimu huo. Tulio wengi tunaufahamu au kwa kusikia au kwa kupitia hapo na kupata huduma mbalimbali za afya.
Kibaha Maili Moja. T-shirts za njano zinatawala. Ni sare kwa ajili ya vijana wanaojishughulisha na biashara ndogondogo pale stendi. Nadhani ni utaratibu mzuri. Ni rahisi kuwatambua. Wao wanafahamiana. Kwa hiyo, ikiwa kuna tukio la uhalifu linatokea pale, basi ni rahisi kufuatilia na kuwapata waliohusika. Pengine miji mingine iige utaratibu huu?
Kazi ya kuboresha Kituo cha Mabasi cha Maili Moja, Kibaha, inaendelea. Tunatarajia kazi bora inayozingatia ukuaji wa magari na watu wanaotumia kituo hicho kwa matumizi mbalimbali. Macho yetu tunayaelekeza hapo. Ni 20 Julai 2008.
Vicious circle of poverty – jamaa anakata miti – anachoma mkaa – anauza – anaganga njaa – miti inakuwa imekwishakatwa – idadi ya miti inashuka – uharibifu wa mazingira – ugumu wa upatikanaji miti ya kuchomea mkaa – kupungua kwa kiwango cha mvua – janga la njaa – hali ngumu zaidi ya maisha kwa vizazi vinavyofuatia. Hatuna budi kutafuta njia za kuzuia chain hii ikiwa kweli tunataka jamii ya Watanzania ipate maendeleo ya kweli. Huyu alipaswa kuwa agent wa kuuza gesi ya songosongo badala ya kuchuuza mkaa. Tunaweza kuleta mabadiliko. Tunaweza kubadili mambo. Hii ni ikiwa tu wawakilishi wetu Bungeni watabeba majukumu yao inavyowapasa, na vivyo hivyo kwetu sisi wengine. Kila mmoja atumie nafasi yake kwa manufaa ya wote.
Katika kipindi hiki cha mwaka, si ajabu kukuta watu wakiota jua la saa 5 hapa jijini Dar. Hapa ni katika bustani iliyo mbele ya NBC HQ, yaani, posta ya zamani.