simbadeo2000

Umeme …

Dec 31
1 Comment

dscf0049.jpg

Kuanzia kesho (bado dakika 20 muda huu ninapoandika) umeme nchini Tanzania utapanda kwa asilimia 22. Ni ongezeko kubwa hasa katika kipindi hiki ambapo thamani ya shilingi imeshuka sana.

Pichani ni wateja waliofurika pale PATCO Supermarket, BP Dar es Salaam International Airport. Niliipiga saa 1.30 usiku, yaani kiasi cha saa 4.30 kabla ya kuingia mwaka mpya 2008. Wateja hawa wameamua kununua umeme leo kwa wingi kabla bei mpya kuanza rasmi hapo kesho tarehe 1 Januari 2008.

 Watu wanazidi kuwa ‘cost conscious’. Yule mlalahoi kama mimi anayenunua umeme wa shilingi 10,000 itampasa kuanza kulipa wastani wa shilingi 12,200 kwa umeme kiasi kilekile. Yeye akienda leo kununua umeme huo haokoi fedha nyingi. Lakini kibopa ambaye matumizi yake ni shilingi 100,000 basi kama alikuwepo kwenye msululu huo aliokoa shilingi 22,000. Unaweza kuona jinsi fedha inavyoanza kuwa kubwa.

Mungu ainusuru Tanzania. Umeme unavyopanda ndivyo bei za bidhaa nyingine nyingi zitakavyopanda. Sasa hivi tutasikia kuwa magazeti bei imepanda. Internet pia itakuwa gharama zaidi. Lo, Mungu tunusuru.


Posted in Uncategorized

Fahari Yetu Inapogeuka …

Fahari Yetu Inapogeuka

Hii ni TAZARA Dar es Salaam. Ni kituo kikuu cha Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia. Ni moja ya miundombinu muhimu kupata kujengwa baada ya UHURU. Kwa mwongo mmoja wa mwanzo tangu kuwapo kwake, hii ilikuwa FAHARI YETU kubwa. Kadiri siku zinavyopita, tunazidi kupoteza FAHARI hii. FAHARI YETU inageuka kuwa AIBU YETU.

Je, tumeshindwa KUJITAWALA? Tumeshindwa Kujiongoza? Kwa nini inapotupasa kuendesha mambo yetu wenyewe MWISHO huwa wazi, KUANGUKA? Kwa nini? Je, jina hili alilowahi kutamka Frantz Fanon: The Wretched of the Earth inaweza kuwa sahihi? Are we the wretched?

Hivi, nani anawajibika kwa hali ambayo TAZARA leo hii imefikia? Nani? Hivi, kwa nini tusimfahamu, akatueleza kuwa ilikuwajekuwaje hata akatutia AIBU hii kubwa? Sidhani kama tuna haja ya kumdai mengi huyu ndugu, ni maelezo tu kwa ufupi kutoka kwake. Hatutamwambia kuwa yale mapesa aliyochota huko aturudishie, hatutamwambia kuwa sasa tunakunyang’anya yale majumba uliyojenga kule Marekani, hatutamwambia kuwa rejesha mapesa yale uliyoweka kwenye akaunti za SIRI kule Uswisi.

Tutamhimiza tu kutupa MAELEZO ya aibu hii, basi. Inatia uchungu sana. Aibu yetu imekaa mahali ambapo kila anayepita anatukebehi nayo. Mgeni. Mwenyeji. Mlaji. Njia panda ya lango la kuelekea DUNIANI. Lango lililopewa jina la shujaa nambari wani wa nchi hii. Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. International Airport.

HUZUNI. AIBU. FEDHEHA.


Posted in Uncategorized

Tunatoka mbali…

10-hour old baby. Martina. Human life is complex. Human life is a mystery. Human life is precious. There is never enough justification to terminate human life. Never. Arbortion is unacceptable. Capital punishment should be stopped once and for all.  The world will be a lot better without the punishment.

Tunatoka mbali. Literally, ‘We come from very far away’, actually meaning ‘we come frome helplessness to full self-freedom’. From a state in which we cannot do without others to a state in which we can do on our own.

Protect life. Give life. Keep life.


Posted in Uncategorized

Merry Christmas 2008

Julius Nyerere

It is 00:47 local time here. It’s Christmas Day. May I wish you a very warm, happy and merry Christmas!

All best wishes during this festive season.

Above is Julius Nyerere International Airport, Dar es Salaam, Tanzania as seen from the front. Hope you enjoy the scenery.


Posted in Uncategorized

Changing face of Dar es Salaam

DDC Kariakoo

Hii ni sura mpya ya DDC Kariakoo, Dar es Salaam. Pamebadilika. Panavutia, tena sana. Biashara inazidi kuchangamka. Bila shaka wawekezaji binafsi waliofungua frame nzuri za kibiashara zimetoa changamoto kwa menejimenti ya DDC kubadili sura ya DDC tuliyozoea kuiona. Hii ni hatua ya kuigwa.

Tatizo, labda ninaloona mimi, je, frame hizi za biashara zitagawiwa/kukodishwa kwa kutumia vigezo gani? Je, zitaishia kwenye mikono ya walewale wa siku zote, WANENE? Je, makundi ya vijana wajasiriamali watapata fursa hapa hata kama wanayo hela ya kulipa kodi inayotakiwa?

Naadhani muda utatupa majibu kwa baadhi au yote ya maswali haya. Tusubiri na kuona.


Posted in Uncategorized

Moon, beautiful face of the moon

Dec 23
1 Comment

Moon, beautiful face of

 Taken 2o minutes ago. Face of the rising moon. Could this symbolize the rising hope for ‘a better year’ that 2008 will become? This is for you and I, this is for Africa, this is for the human species. Is 2008 going to be a better year for us all? Is the crisis in Darfur going to be resolved? Is there going to be peace in all war-torn parts of the world? The Congo, Burundi, Somalia, Iraq, Afghanistan, Myanmar (Burma)?

This is to wish you all best wishes for the New Year 2008. This is to challenge you so that you will be part of those factors needed to make the coming year ‘a better’ year than the previous ones. Change begins with YOU and I. Yes we can. We can change things and situations for the better for humanity.


Posted in Uncategorized

Dec 22
1 Comment

Additions to Dar es Salaam City

Hizi ni nyongeza nyingine muhimu katika sura ya Jiji la Dar es Salaam. Jengo lenye column ya blue ni la Utumishi, na ile nguzo kule mbele ni Nguzo ya kuongozea meli wakati zinaingia au kutoka bandarini Dar es Salaam.

Ama kwa hakika Dar inachukua sura mpya. Laiti hali hii ingejidhihirisha pia katika maisha ya Watanzania wa kawaida, ingependeza zaidi.

Wadau mna mawazo gani?


Posted in Uncategorized

Piracy

Dec 22
1 Comment

Piracy

A cool message.

Hivi karibuni kulikuwa na taarifa katika vyombo vya habari kuhusu bidhaa feki zinazoingizwa nchini na kusambazwa madukani. Baadhi ya bidhaa hizo zilikamatwa na kuteketezwa na mamlaka zenye majukumu ya kudhibiti ‘uharamia’.

Uharamia bidhaa una hatari nyingi. Kwanza, bidhaa hizo hazikidhi viwango vya ubora vinavyohitajika kwani havipitii katika mamlaka zenye jukumu la kupima na kukagua ubora huo. Pili, bidhaa hizo huhujumu ‘jasho’ la wale waliozibuni na kuingia gharama (kwa maana zote) za awali za maandalizi mpaka kutoa bidhaa inayohusika. Tatu, kujishughulisha na bidhaa feki zinazotokana na uharamia ni uhalifu. Nne, bidhaa feki zinachangia katika kudunisha maendeleo ya nchi katika nyanja za sayansi, teknolojia na maendeleo kwa ujumla, kwani bidhaa hizi huua ubunifu (maana wabunifu hukatishwa tamaa kuwa kile watakachobuni hawatanufaika nacho kwani baada ya muda kitakuwa kimeibwa na kuwanufaisha wengine).

Uharamia unaathiri karibu kila kazi ya ubunifu: kazi za sanaa kama vile za uchoraji, uchongaji, muziki; kazi za utunzi na uchapishaji wa vitabu; ubunifu wa mitindo ya mavazi; kazi za ugunduzi/uvumbuzi wa kisayansi na nyinginezo nyingi.

 Ndiyo maana utasikia kuwa kuna vitabu feki, dawa feki, vinyago feki, na bidhaa nyingine nyingi ambazo ni feki.

Tufikishiane ujumbe huu: Uharamia ni uhalifu. Acha kujihusisha na uharamia.


Posted in Uncategorized

Enigma

Enigma

Flower. Concrete. Wood. Air. Life. Soil.


Posted in Uncategorized

Barabara na nishati ya umeme

Barabara na nishati ya umeme

 Ndiyo, ili tuendelee, tunahitaji pia barabara bora na nguvu za umeme za uhakika.

Hapa ni Kinyerezi, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaa, Tanzania. Picha imepigwa mwezi Desemba 2007.


Posted in Uncategorized
Next Page »

About author

I am a citizen of Tanzania. I live in Dar es Salaam, commercial city of Tanzania. I am an editor, particularly dealing with books as well as other publications and related activities: editing, translating, supervising design and layout, monitoring printing, warehousing and dissemination of the books. I am also an author: I write children's story books, school textbooks and adult books. I undertake translation tasks from English to Kiswahili and vice versa. I do book indexing, that is preparing an index for a professional book. Contact: kakasimba@gmail.com . Feel free to get in touch with me.

Search

Navigation

Categories:

Links:

Archives:

Feeds