Jamani tumpe support Bob Sankofa katika kinyang’anyiro cha Zafaa huko UK kwa kumpa kura zetu. Bado nafasi ya kufanya hivyo ipo mpaka tarehe 6 Oktoba mwaka huu. Bonyeza kivyako.
Wito wake ni huu:
PIGIA KURA FILAMU YA “PLAY YOUR PART”
Juzi niliandika kuwa filamu yangu ya “PLAY YOUR PART” imependekezwa kuwa moja ya filamu zinazoshindania tuzo kubwa kabisa ya filamu za sinema Afrika, tamasha linafanyika London. Tafadhali bonyeza hapa usome habari ile. Kwa bahati nzuri siku hizi mambo yamebadilika sana, wanaochagua mshindi wa tuzo ile ni watu kama wewe amabo wanapiga kura kuichagua filamu wanayotaka ishinde tuzo ile.
Hivyo basi, ninakuomba wewe mdau wa blogu hii ubonyeze hapa halafu kwenye ukurasa ule kuna kundi linaitwa “BEST DOCUMENTARY FEATURE” pale utaiona filamu ya “PLAY YOUR PART” amabyo hadi sasa ndiyo yenye kura nyingi zaidi ya filamu shindani toka Zambia na Uganda.
Naomba uipigie kura “PLAY YOUR PART” kabla giza halijaingia na unisaidie kumwambia na rafiki yako apaige kura pia ili Filamu na Tanzania vitoke kimasomaso. Endelea kupiga kura kila siku hadi tarehe 6/10. Asante.
PAMOJA!
Picha iliyo pale juu kwa hisani ya: http://mjengwa.blogspot.com/