simbadeo2000

Kwa nini niwe wewe?

Kila mtu ni yeye, hakuna anayeweza kuwa mwingine badala ya yeye. Niache nilivyo, acha niwe mimi.

Mimi ni Bondia 

Mimi ni bondia,

Bondia, ndia, ndia

Bondia. 

Nipo ulingoni,

Lingoni, ngoni, ngoni,

Ulingoni. 

Mimi ni bondia,

Nipo ulingoni,

Bondia ulingoni. 

Mpinzani wangu kivuli,

Ushindani honekani,

Ni hewa. 

Nipo ulingoni,

Na kamba za mikononi,

Kamba. 

Nipo ulingoni,

Na kamba za miguuni,

Kamba. 

Nafanya jitihada,

Kupambana na ushindani,

Umaskini tokomeza. 

Mimi ni Machinga,

Napambana na Wamanga,

Kote kote wanakaba. 

Mimi ni Mkulima,

Napambana na ruzuku,

Majuu wanapewa ruzuku. 

Kamba za mikononi,

Ntatupa ngumi vipi?

Nauliza. 

Kamba za miguuni,

Ntakwepa masumbwi vipi?

Hebu jibu. 

Mpinzani wangu yu huru,

Abebwa na soko huria,

Twakabiliana sokoni, ulingoni.

Ngumi zaingia puani,

Nyingine natua kichwani,

Uso wote mevimba, kamba mikononi. 

Natumia nguvu nyingi,

Mashambulizi kuyakwepa,

Nifurukutie wapi? 

Mimi ni bondia,

Mimi ni Machinga,

Ulingoni natwangana. 

Mimi ni Mkulima, mteja,

Nipo ulingoni,

Saa zote nipo ulingoni. 

Mimi ni mimi,

Kamba mikononi,

Sitaacha kupambana. 

Naungana na Machelli,

Aluta continua nasema,

Aah, aluta continua. 

Nyerere naye Lumumba,

Mapambano endeleza,

Utu wetu kuupata. 

Mimi ni mimi,

Nataka kuwa mimi,

Sitaki kuwa wewe.   

Simba Deogratias

Dar es Salaam,

Agosti 2007 


Posted in Uncategorized

About author

I am a citizen of Tanzania. I live in Dar es Salaam, commercial city of Tanzania. I am an editor, particularly dealing with books as well as other publications and related activities: editing, translating, supervising design and layout, monitoring printing, warehousing and dissemination of the books. I am also an author: I write children's story books, school textbooks and adult books. I undertake translation tasks from English to Kiswahili and vice versa. I do book indexing, that is preparing an index for a professional book. Contact: kakasimba@gmail.com . Feel free to get in touch with me.

Search

Navigation

Categories:

Links:

Archives:

Feeds