simbadeo2000

Shukrani

Lengo la post hii ni kutaka kutoa shukrani kwa Bw Ndesanjo kwa kujulisha kuhusu njia hii ya mawasiliano ya 'blogu'. Vile vile shukrani hizi ziwafikie watu wa gazeti la Kiswahili la Mwananchi kwa kuchapisha makala za Bw Ndesanjo, ambako kwa kweli ndiko ambako watu wengi, kama mimi, tumepata kujua kuhusu teknolojia hii ya mawasiliano.

 Binafsi, tangu niliposoma makala zile miezi kadhaa iliyopita, kama inavyoeleweka kwa wengi hapa Tanzania, sikufaulu sana kufuatilia kwa karibu namna gani blogu zinafanya kazi. Sababu moja ni matatizo ya kasi ya huduma za Internet hapa Tanzania. Ni katika migahawa michache sana ambapo mtu utapata fursa ya kupiga mbizi katika mtandao kwa kasi ya kuridhisha.

 Lakini pia kuna suala la muda na gharama. Tumekuwa tukikimbizana na maisha kiasi kwamba mtu unakosa muda kabisa wa kukaa kwenye mgahawa wa mtandao ili kupiga mbizi humo japo kwa saa moja. Mara nyingi watu wanatumia nusu saa ili kutazama barua pepe zao, kujibu na labda kuandika nyingine. Muda wa kukaa kuanza kuandika makala ndefu tena iliyotulia linakuwa jambo gumu.

 Pamoja na hayo, habari ni habari, na ufahamu wa habari fulani unampa mtu nguvu, nguvu ambayo mtu anaweza hata kuitumia kujiletea kipato/maarifa zaidi.

 Kwa hiyo, shukrani nyingi kwa Bw Ndesanjo na Gazeti la Mwananchi. Asanteni sana pia kwa utayari wenu wa kusaidia wale wenye matatizo ya kutumia teknolojia hii. Mimi ni mmoja wapo, mtanisikia kila ninapokwama.

 Kila la kheri.


Posted in Uncategorized

Hello world!

Welcome to WordPress.com. This is your first post. Edit or delete it and start blogging!


Posted in Uncategorized

About author

I am a citizen of Tanzania. I live in Dar es Salaam, commercial city of Tanzania. I am an editor, particularly dealing with books as well as other publications and related activities: editing, translating, supervising design and layout, monitoring printing, warehousing and dissemination of the books. I am also an author: I write children's story books, school textbooks and adult books. I undertake translation tasks from English to Kiswahili and vice versa. I do book indexing, that is preparing an index for a professional book. Contact: kakasimba@gmail.com . Feel free to get in touch with me.

Search

Navigation

Categories:

Links:

Archives:

Feeds